Thursday, September 24, 2015

VIDEO: Maneno ya EDWARD LOWASSA Kama Atakubali au Atakataa Matokeo Akitangazwa AMESHINDWA


ZIKIWA  zimebakia  siku 30  kabla  watanzania  hawajapiga  kura  ya  kumchagua  Rais,mgombea  urais  kwa  tiketi  ya  CHADEMA, Edward  Lowassa  ambaye  amekuwa  akieleza  imani  yake  kuwa  atashinda  kwa  kishindo, ameeleza  msimamo  wake  endapo  tume  ya  Taifa  ya  Uchaguzi  itatangaza  matokeo  tofauti  na  ya  matarajio  yake.

Akiongea  na  kituo  cha  Runinga  cha  Citizen  cha  nchini  Kenya, Lowassa  amesema  hawezi  kusema  kama  atakubali  au  atakataa  hadi  itakapothibitika  kuwa  matokeo  hayo  hayajahujumiwa.

"Siwezi  sema  nitakuchukulia  kama  nimeshindwa  hadi  nitakapothibitishiwa  kuwa  kila  kitu  kimeenda  sawa  na kwamba  hakuna  hujuma." Alisema  Lowassa  na  kuongeza;

"Tunaogopa  sana  kuhusu  hujuma.Kila  mtu  unayeongea  naye  unapokutana  naye, anakwambia  utashinda, lakini  je, watakubali  kushindwa?"

Katika  hatua  nyingine,Lowassa  alijibu  swali  la  mwandishi  lililomtaka  kueleza  kama  angeweza  kusema  anachokisema  hivi  sasa  kuhusu  CCM  endapo  angechaguliwa  kuwa  mgombea  Urais  kwa  tiketi  ya  CCM.

"Ninasema  vitu  vingi  ambavyo  vingeweza  kufanywa  vizuri  zaidi  na  CCM,na  ninasema  vitu  vingi  ambavyo    ninaweza  kuvifanya  vizuri  zaidi  nikiwa  Upinzani."  alisema  Lowassa.
 Tazama  Video  Hapo  Chini  kumsikiliza

Wednesday, September 23, 2015

Baada ya TWAWEZA kusema CCM inakubalika 66 %, haya ni maneno 15 ya Lowassa na 26 ya Zitto Kabwe

Kuelekea uchaguzi mkuu October 25 2015 matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA yametolewa September 22 2015 Tanzania na kuonyesha Watanzania mbalimbali wanamkubali nani zaidi ambapo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%, C.U.F 1%, ACT 0%, NCCR 0%, UKAWA 3%.
Baada ya utafiti huu kutoka chumba cha habari kilipitia page za Twitter za Wagombea Urais na vyama vyao kutazama kama kuna walichoandika baada ya kupata haya matokeo.
Mgombea Urais Edward Lowassa ambaye yuko kwenye tiketi ya CHADEMA ameyaandika haya kwenye page yake halali ya Twitter >>> ‘Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki, tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata
 Dr John Magufuli @MagufuliJP
Wananchi wa Bukoba nimefarijika pasipo na wasiwasi kwa namna mlivyojitokeza kwa wingi kukiunga Chama Cha Mapinduzi. 
 
Kuelekea uchaguzi mkuu October 25 2015 matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA yametolewa September 22 2015 Tanzania na kuonyesha Watanzania mbalimbali wanamkubali nani zaidi ambapo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%, C.U.F 1%, ACT 0%, NCCR 0%, UKAWA 3%.
Baada ya utafiti huu kutoka chumba cha habari kilipitia page za Twitter za Wagombea Urais na vyama vyao kutazama kama kuna walichoandika baada ya kupata haya matokeo.
Mgombea Urais Edward Lowassa ambaye yuko kwenye tiketi ya CHADEMA ameyaandika haya kwenye page yake halali ya Twitter >>> ‘Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki, tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata
Dr. Magufuli hakuwa ameandika chochote kuhusu utafiti huu huku tweet yake ya mwisho ikiwa inaeleza furaha yake kwa jinsi Wananchi wa Bukoba walivyojitokeza kumsikiliza.
Kwa upande wa ACT Wazalendo, kiongozi wake Zitto Kabwe aliandika kwenye Twitter ‘Chama chetu kinaamini kwenye tafiti haijalishi zina matokeo mazuri au mabaya kutuhusu, tumepokea matokeo haya kama changamoto… tutaongeza nguvu yetu kuhakikisha tunapata asilimia zaidi kwenye kura’
Kingine alichosema Zitto ni >>> ‘Ikumbukwe kwamba utafiti huu wa TWAWEZA umefanywa kabla ya chama cha ACT WAZALENDO hakijapata mgombea Urais na kabla ya uzinduzi vilevile

Tuesday, September 22, 2015

CHADEMA Wachangisha Milioni 97 za Kampeni...... Mbowe Asema Wako Matajiri Watano Ambao Wameapa Kukipigania Chama


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama chake kina watu watano wenye uwezo wa kiuchumi wanaoweza kukisaidia chama hicho kuendesha shughuli zake za kampeni, ikiwa ni siku 32 kabla ya wananchi kupiga kura Oktoba 25.

Picha na Video ya Magufuli Akipiga Push-Up Kuonesha Yuko FITI


Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akipiga 'push-up' kuonesha kuwa anauwezo wa kufanya kazi ukilinganisha na wagombea wengine.

VIDEO: Chadema Yamvaa Bulembo Aliyesema CCM Haiko Tayari Kukabidhi IKULU Kwa Wapinzani


KAULI ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo kwamba “CCM haitafanya makosa kukabidhi Ikulu kwa wapinzani” imezua mjadala.

Bulembo alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kampeni za urais wa mgombea wa chama chake Dk. John Magufuli Kigoma.

“Serikali imefanya makosa mengi na Chama Cha Mapinduzi kimefanya makosa mengi lakini hakitofanya kosa la kuruhusu chama pinzani kuingia Ikulu,” alisema Bulembo.

Emmanuel Mbasha Aachiwa Huru...Upande wa Mashtaka Umeshindwa Kuthibitisha kosa la Ubakaji dhidi yake


Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Emmanual Mbasha (32), leo ameangua kilio baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Ilala huku mke wake, Flora amesema yuko tayari warudiane endapo ataomba radhi. Mbasha alimwaga chozi muda mfupi baada ya kutoka katika chumba cha Mahakama alipopandishwa kizimbani kusomewa hukumu. Mshtakiwa huyo ameachiwa huru dhidi ya kesi ya ubakaji iliyokuwa...

MAFURIKO Ya Lowassa Jana Jijini Dar es Salaam

Lowassa jana aliendelea na kampeni zake katika majimbo matatu ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ni Ukonga, Kigamboni na Mbagala. Hizi  ni  Picha  Za  Maelfu  ya  Wananchi  waliofurika  Kumsikiliza

Popular Posts