Sunday, August 9, 2015

Hili Hapa Goli la Simba Vs SC Villa Aug 8 2015 ( Simba Day)

Simba DayTimu ya Simba SC leo imefanikiwa kuibuka na ushinda wa goli 1-0 kwenye mchezowake wa kirafiki dhidi ya timu ya SC Villa ya Uganda mchezo uliokuwa maalumu kwa ajili ya kusherekea siku ya Simba Day ambayo huadhimishwa Agosti 8 kila mwaka.
Simba Day 3Goli la Simba limefungwa na Awadh Juma dakika za lala salama baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Villa ‘Jogoo’ hatimaye mpira kumkuta Awadh aliyeachia huti kali na kuipa timun yake ushindi wa jioni
Simba Day 2Awali washambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu, Mussa Hassan Mgosi na Hamisi Kiiza walipoteza nafasi nyingi za kufunga kutokana na nafasi nyingi zilizotengenezwa.
Hata hivyo kikosi cha Villa kiliruhusu goli hilo baada ya kucheza pungufu kwa muda mrefu kuokana na mchezaji wao Yeberi Waibi kuoneshwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha kwanza kwa kumchezea rafu Ibrahim Ajibu wa Simba hivyo kukifanya kikosi chake kicheze kikiwa pungufu kwa muda wote uliobaki.
Simba Day 4Kipindi cha kwanza kilimalizika bila timu hizo kufungana, kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hatimaye mabadiliko yakazaa matunda kwa upande wa Simba bada ya Awadh kuifungia goli timu yake akitokea kwenye benchi.
Hiyo ni mechi ya sita ya kirafiki (zote imeshinda) kwa  upande upande wa Simba ambapo mechi nyingine tano ilicheza wakati ipo visiwani Zanzibar ilipokuwa imeweka kambi kwa maandalizi ya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts