Friday, September 4, 2015

JAFFARI MNEKE ATOA TANGAZO MAALUM KWA WANACHAMA WOTE WA UKAWA..NI MUHIMU SANA LISOME

Bw. Jaffar Mneke akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi huo wa kampeni zake za ubunge huko Newala jijini Dar es Salaam Jana


Mgombea ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Jaffar Mneke (PICHANI) kwa jimbo la Newala Vijijini anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), atazindua kampuni zake Jumapili Septemba 06, 2015 katika viwanja vya Kitangari Sokoni mjini Kitangari.
Akizungumza jana (Alhamisi) jijini Dar es Salaam, Bw. Mneke amesema uzinduzi huo utakaohudhuriwa na mamia ya wananchi waliotayari kwa mabadiliko utafanyika katika viwanja hivyo kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 12 jioni.
Aliongeza kuwa viongozi kadhaa wa kitaifa wa vyama vya Ukawa, mkoa na wilayani watahudhuria uzinduzi huo nitakaoutumia pia kutambulisha kauli mbiu inayochagiza mabadiliko kwa wana Newala isemayo “Safari ya Mabadiliko ya Kweli Newala.”
“Nitautumia mkutano huo kueleza ilani ya Ukawa katika kuwaletea wananchi wa Tanzania na Newala mabadiliko lakini pia kama mgombea makini wa jimbo hilo nitaeleza tatizo kubwa linalokwamisha maendeleo ya jimbo na kuwataka wananchi waubngane nami katika safari ya mabadiliko na kujikomboa kutoka katika tanuru la umaskini, kero zisizokwisha na maendeleo duni,” alisema.
Katika uzinduzi huo pia wananchi mbalimbali watapata fursa ya kuainisha kero za muda mrefu wanazotaka Serikali na Mbunge wa Ukawa wazifanyiekazi.
Bw. Mneke ambaye kitaaluma ni mwalimu na mwanadiplomasia anasema alipata elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St. John’s University of Tanzania) ambako alitahasusi katika masuala ya Elimu na kutunukiwa shahada ya kwanza ya Uwalimu.

Kati ya mwaka 2013 na 2014 alijiunga na Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam na kujipatia Stashahada ya Umahiri katika Diplomasia (Post-Graduate Diploma in Management of Foreign Relations) ambako alihitimu kwa kiwango cha mwanadiplomasia wa daraja la kwanza (first class)
Amewaambia wanahabari kuwa pamoja na kazi mbalimbali za harakati za kuchagiza maendeleo katika ngazi ya Taifa na kimataifa, kwa miaka kadhaa amefanyakazi adhimu ya ualimu ambako alipanda ngazi hadi kuwahi kuwa Makamu Mkuu wa Shule katika Shule za Sekondari za Ilala na Dar es Salaam Islamic.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts