Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Kiuchezaji anaendana na winga Mholanzi, Arjen Robben ama Mhispani Jesus Navas. Namzungumzia mshambuliaji hatari kijana raia wa Nigeria ambaye ataambatana na kikosi cha timu yake ya taifa kuja nchini kucheza na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Akiwa na miaka 23 sasa hivi, Amhed Musa ameifungia ‘Super Eagle’magoli 10 katika mechi 48 tangu alipoitwa kikosi kwa mara ya kwanza mwaka 2010. Musa ndiye mchezaji pekee wa Nigeria kufunga mara mbili katika mechi moja ya kombe la dunia. Alifanya hivyo wakati Nigeria ilipofungwa 3-2 na Argentina katika michuano iliyopigwa Brazil 2014.
Musa alizaliwa October 14,1992 na amechezea timu za taifa za vijana za Nigeria U20 & U23 mwaka 2011 alirushwa hadi timu ya taifa angali na miaka 18 mwaka 2010 ni mchezaji mwenye kasi. Musa ana uwezo mkubwa wa ‘ kudribbling’ atakuwa tatizo kubwa kwa walinzi wa Stars.
Walinzi wa stars watatakiwa kuepuka kumfanyia faulo maeneo ya hatari kwa kuwa ni mchezaji mjanja sana wa kutafuta penalti. Miaka minne aliyocheza barani ulaya kijana huyo amecheza jumla ya gemu 132 na sasa ndiye nyota wa kutegemewa katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi. Amefunga magoli 31 katika gemu 102 akiwa Urisi.
Musa alifunga magoli 18 katika msimu wake wa kwanza katika ligi ya Nigeria wakati alipoisaidia Kano Pillars FC kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 2009. Ilikuwa idadi ya juu zaidi ya mfungaji bora katika ligi ya Nigeria. Akaivunja rekodi hiyo mwaka uliofuata baada ya kufunga mabao 20.
Barani Ulaya alikwenda angali na miaka 17 lakini FIFA ikampa ruhusa ya kuanza kuichezea VVV-Venilo ya Uholanzi Oktoba 14,2010 mara baada ya kufikisha miaka 18. Alicheza gemu 37 na kufunga mabao 8 akiwa Uholanzi.
Musa ni mshambulizi mkali kwa sasa wa kinigeria na mwalimu, Sunday Oliseh atamtumia kama silaha yake muhimu katika gemu yake ya kwanza akiwa kama kocha na si mchezaji wa Super Eagles. Makosa kidogo kwa walinzi wa pembeni yataigharimu Stars kwani Musa ni mchezaji hatari hasa anapotokea katikati ya uwanja.
No comments:
Post a Comment