Friday, August 14, 2015

USIPITWE NA HAYA YANAYOENDELEA NDONDO CUP UPANDE WA USHANGILIAJI

Makumba vs Temeke 18Michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup inayodhamniwa na Dr. Mwaka kwa kushirikiana na kampuni ya Azam Food Products inaendelea kuchukua sura mpya kila kukicha lakini kikubwa ni burudani mbalimbli zinazopatikana uwanjani wakati mechi zikiendelea.
Makumba vs Temeke 15Mbali na burudani ya soka safi kutoka kwa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, nje ya uwanja kunaburudani nyingine inayotolewa na vikundi vya ushangiliaji vinavyokuja uwanjani kwa ajili ya kuzishangilia timu zao zinapokuwa zinamenyana uwanjani.
Makumba vs Temeke 17Jana kwenye uwanja wa Bandari, Tandika, kulikuwa na mechi kati ya Makumba FC dhidi ya Temeke Market mchezo uliomalizika kwa Makumba kushinda mchezo huo kwa goli 1-0 lililofungwa na Idd Mwalala kwa mkwaju wa penati. Kubwa zaidi katika mchezo huo ni mashabiki wa Makumba FC walivyofunika kwa kuishangilia timu yao tangu dakika ya kwanza mpaka filimbi ya mwisho.
Makumba vs Temeke 12
Leo shughuli itahamia uwanja wa Karume, Ilala ambapo Friends Rangers itakuwa ikichuana na Goms United kwenye mwendelezo wa hatua ya 16 bora.
Makumba vs Temeke 10
Makumba vs Temeke 7
Makumba vs Temeke 9
Makumba vs Temeke 6
Idd Mwalala (katikati) akipongezwa na wadada wa timu ya ushangiliaji ya Makumba FC baada ya kuifungia goli timu hiyo
Idd Mwalala (katikati) akipongezwa na wadada wa timu ya ushangiliaji ya Makumba FC baada ya kuifungia goli timu hiyo

No comments:

Post a Comment

Popular Posts