Mchezaji Mbaruku Chande wa JKU
aliifungia goli la kwanza timu yake dakika ya 32 kipindi cha kwanza huku
bao la pili likifungwa na Hamisi Said dakika ya 72 kipindi cha pili.
Katika mchezo huo, Simba
imewachezesha wachezaji wake wawili wa kimataifa kutoka Mali na Senegal
wanaofanya majaribio kwenye timu hiyo ili mmoja wao kama atamvutia kocha
na benchi zima la ufundi asajiliwe kwa ajili ya msimu ujao.
Baada ya kipigo hicho kocha wa
Simba Dylan Kerr alimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo kwa kitendo cha
mwamuzi huyo kumkatalia kumuingiza mchezaji ambaye alishacheza akatolewa
kupumzika kisha kocha huyo akataka kumuingiza tena uwanjani kwa madai
kwamba walikuwa wamekubaliana kabla ya mchezo kuanza.
No comments:
Post a Comment