Saturday, August 29, 2015

AZAM YATUNISHIWA MSULI NA NDANDA, YABANWA MTWARA

????????????????????????????????????
Azam ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Kelvin Friday lakini Ndanda walisawazisha goli hilo dakika ya 80 kipindi cha pili.
Stephen Mwantika wa Azam FC alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 70 baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Ndanda ndani ya eneo la hatari na mwamuzi akaamuru ipigwe penati lakini mpigaji wa penati hiyo alipaisha mpira.
Kesho Azam inarejea jijini Dar es Salaam wachezaji watapumzika siku ya Jumatatu, Jumanne watashuka tena dimbani kukipiga dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts