Sunday, August 30, 2015

MAN U YAPITA NJIA YA LIVERPOOL NA CHELSEA, YAKIONA CHA MOTO MBELE YA SWANSEA

Gomis akishangilia goli lake
Gomis akishangilia goli lake
Manchester United imeshindwa kutamba mbele ya Swansea City kwenye mchezo wa ligi kuu England (EPL) baada ya kukubali kipgo cha goli 2-1 kwenye mchezo uliomalizika usiku huu.
Manchester ndio walikuwa wa kwana kupata goli kupitia kwa Juan Mata dakika ya 48 kipindi cha pili akiunganisha pasi kutoka kwa Luke Shaw lakini bao hilo halikuumu kwani dakika ya 61 Ayew aliisawazishia Swansea na kuufanya mchezo kuwa sare kwa goli 1-1.
wachezaji wa Manchester wakishangilia goli liliofungwa na Mata
wachezaji wa Manchester wakishangilia goli liliofungwa na Mata
Gomis akaipa ushindi Swansea kwa kuifungia goli la pili dakika ya 66 na kuifanya timu yake ichomoke na pointi tatu muhimu kwenye uwanja wa nyumbani Liberty Stadium.
Man U inakuwa kigogo cha tatu kupoteza mchezo wake bada ya jana Chelsea na Liverpool kubanwa mbavu na kupokea vipondo kwenye mechi zao.
Gomis akitembea kama nyani mara baada ya kuifungia Swansea goli la pili
Gomis akitembea kama nyani mara baada ya kuifungia Swansea City goli la pili

No comments:

Post a Comment

Popular Posts