Wachezajio wa Yanga wakisherekea ubingwa wa Ngao ya Jamii waliuotwaa mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Mabingwa wa kandanda Tanzania
bara, Yanga SC wamewasilisha majina ya wachezaji 24 kwa Shirikisho la
soka nchini TFF. Wachezaji 7 wa kigeni na wengine 17 wa ndani
waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya michezo ya ligi kuu msimu huu,
kombe la FA na michuano ya klabu bingwa barani Afrika mapema mwakani.
Kwa zaidi ya miaka kumi sasa
mabingwa hao mara 24 wa kihistoria wa Tanzania bara walikuwa na
‘kasumba’ ya kusajili wachezaji zaidi ya 26-30 lakini mwalimu Hans Van
der Pluijm ameridhika na wachezaji waliopo katika timu huku pia
akitaraji kuwatumia wachezaji wa kikosi cha vijana katika baadhi ya
michezo.
Wachezaji ambao majina yao yamewasilishwa TFF ni;
Makipa: Benedict Tinocco, Mudathir Khamis, Deogratius Munishi na Ally Mustafa.
Walinzi: Juma Abdul, Pato Ngonyani, Kelvin Yondan, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Mwinyi Haji Mngwali.
Viungo: Salum Telela, Said Juma
Makapu,Geofrey Mashuiya, Deus Kaseke, Saimon Msuva. Washambuliaji: Malim
Busungu, Mateo Anthony Simon.
Achezaji saba wa kigeni ni:
Vincent Bossou (Togo) , Donald Ngoma, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Mbuyu
Twite, Haruna Niyonzima (Rwanda), Andrey Coutinho (Brazil) na Amis
Tambwe (Burundi)
No comments:
Post a Comment