Wednesday, August 26, 2015

OLUNGA ATUA AFRIKA KUSINI KWA MAJARIBIO KWENYE TIMU ILIYOWATEMA MSUVA NA MKUDE

Mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya Michael Olunga
Mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya Michael Olunga
Mshambuliaji tegemezi wa Gor Mahia, Michael Olunga yupo nchini Afrika Kusini akifanya majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits inayoshiriki ligi kuu ya nchini hiyo (PSL).
Olunga alisafiri Jumatatu kuelekea kwa Madiba kujaribu bahati yake kufuatia msimu mzuri alikuwanao kwenye ligi ya Kenya (Kenyan Premier League) ambapo amekuwa akiifungia timu yake magoli muhimu.
Akizungumza kupitia supersport.com akiwa Geneva, mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amethibitisha kuwa kunamaendeleo mazuri juu ya dili hilo.
 “Tumempa ruhusa Michael Olunga kusafiri kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits baada ya klabu hiyo kuwatumia maombi ya kumhitaji Olunga kwenda kufanya majaribio”, amesema Rachier.
 “Bado ni mchezaji wetu hadi 2016 na tutahusika moja kwa moja kwa lolote litakalotokea. Atakuwa huko kwa wiki moja na tumewapa baraka zetu, Rachier aliiambia supersport.com”.
Olunga anakuwa mchezaji wa pili kufanyiwa majaribio kwenye klabu ya Bidvest ndani ya kipindi cha wiki moja akimfuata mfungaji anaeongoza kwa kupachika mabao kwenye ligi ya Kenya akiwa ameshafunga mabao 19 lakini akashindwa kumshawishi kocha wa Wits Gavin Hunt.
Olunga pia alitwaa kiatu cha dhahabu kwenye michuano ya CECAFA Kagame baada ya kutupia nyavuni goli tano lakini timu yake ikashindwa kuchukua kombe hilo ilipokubali kipigo cha goli 2-0 kwenye fainali ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts