Saturday, August 22, 2015

NAY WA MITEGO, PAM D WAFANYA UCHAFU KWENYE GARI


Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
OHOOO! Wasanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mwanadada Pamela Daffa ‘Pam D’ wamenaswa wakidendeka ndani ya gari la Nay aina ya Nissan Murano.
Tukio hilo lililonaswa ‘live’ na makachero wetu, lilijiri hivi karibuni usiku, maeneo ya Kinondoni Studio jijini Dar ambapo makachero wetu walikuwa wakirandaranda mitaani kusaka matukio ndipo wakakutana na tukio hilo la aibu.
Mapaparazi wetu baada ya kulibaini gari aina ya Murano ni la Nay na limepaki uchochoroni huku ndani akiwa na mrembo huyo wakifanya madudu yao, waliwasogelea kwa staili ya kunyata na walipowakaribia, walipiga picha fasta kisha kutoweka eneo hilo.
Baada ya kujiridhisha kuwa Nay alikuwa na Pam D kupitia picha hiyo, siku iliyofuata mapaparazi wetu walianza kumtwangia simu Pam D anayetamba na ngoma ya Popolipopo ambaye alishtuka kuambiwa picha hiyo imenaswa.
 “Daah! Kumbe mlionipiga picha ni nyinyi? Aisee nimewavulia kofia, lakini kwani tatizo liko wapi mimi kuwa na Nay kwenye gari na kufanya yale tuliyoyafanya?,” aliwahoji mapaparazi wetu Pamela na kukata simu.
Alipotafutwa Nay, alijibu kwa kifupi: “Niko taiti kidogo nipigie baadaye.”
Alipopigiwa tena baadaye, hakupokea.
Nay baada ya kumfumania mzazi mwenzake Siwema miezi kadhaa iliyopita kisha kuachana naye, alizama kwenye ‘malovee’ na staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford ambapo naye hivi karibuni alidai wameachana na hatimaye amenaswa na Pam D.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts