Friday, August 28, 2015

KIMWAGA: “NILIANZA KUKATA TAMAA YA KUCHEZA SOKA….”

Kiungo wa Simba SC Joseph Kimwaga akiwa chini baada ya kupata maumivu wakati timu yake ilipocheza mchezo wa kirafiki dhiddi ya Mwadui FC
Kiungo wa Simba SC Joseph Kimwaga akiwa chini baada ya kupata maumivu wakati timu yake ilipocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam 
Kiungo anaekipiga kwa mkopo katika klabu ya Simba SC, Joseph Kimwaga amekiri wazi kuwa alikata tama ya kucheza mpira baada ya mambo kuwa magumu katika klabu ya Azam FC. Kimwaga licha ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Azam FC alisumbuliwa na majeraha ya goti kiasi cha kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.
Mchezaji huyo anayertumia mguu wa kushoto anakumbukwa na wapenzi wengi wa mpira nchini kutokana na kufunga goli la ushindi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC Novemba, 2013 wakati Azam iliposhinda 3-2.
“Baada ya kuumia na kuwa nje kwa muda mrefu nilianza kukata tama kama kweli ningeweza kurudi katika kiwango changu cha kawaida. Kusajiliwa na Simba nitachukulia kama njia ya kurejesha makali yangu” anasema Kimwaga wakati nilipozungumza naye kwa njia ya simu akiwa kambini Zanzibar.
Kimwaga 1Simba imekuwa Zanzibar kwa kambi ya mwisho kabla ya kuanza kwa ligi kuu Septemba 12, itacheza na JKU ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki siku ya Jumapili hii. Kimwaga tayari amecheza gemu moja ya maandalizi wakati timu hiyo ilipotoka sare ya bila kufungana na Mwadui FC wiki iliyopita anatajwa kama mtu wa kuchukua nafasi iliyoachwa na winga Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye amejiunga na Azam FC.
“Nipo hapa kufanya kazi, lengo langu ni kushirikiana na wenzangu kuisaidia Simba msimu huu. Najifua ili kumshawishi mwalimu nipate nafasi ya kucheza mara kwa mara. Unajua nimekuwa nje ya uwanja kwa mwaka mzima kutokana na majeraha. Anasema Kimwaga ambaye tangu amepona hakuwahi kuichezea Azam FC katika gemu ya ushindani.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts