Wednesday, August 19, 2015

HII NDIO RATIBA YOTE YA VPL MSIMU WA 2015-2016

YANGA BINGWARatiba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) imetoka leo ambapo jumla ya timu 16 zinashiriki ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Septemba 12 katika viwanja tofauti nchini na kumalizika Mei 7, 2016.
TFF inavisisitiza vilabu kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usjaili kesho siku ya Alhamisi Agosti 20, 2015. Baada ya kufungwa kwa usajili huo hakutakuwa na muda tena wa nyongeza.
Kwa klabu ambayo haitawasilisha malipo ya ada ya mchezaji wa kigeni ya dola elfu mbili (U$D 2000) mchezaji huyo hataruhusiwa kucheza kwenye ligi hadi malipo hayo yatakapofanyika. 
Michezo saba itachezwa siku ya ufunguzi Juma
mosi Septemba 12 katika viwanja tofauti ambapo mechi zitakuwa kama ifuatavyao; Ndanda Vs Mgambo Shooting (Nang’wanda – Mtwara), African Sports Vs Simba SC (Mkwakwani – Tanga), Majimaji Vs JKT Ruvu (Majimaji – Songea), Azam FC Vs Tanzania Prisons (Azam Complex – Dsm), Stand United Vs Mtibwa Sugar (Kambarage – Shinyanga), Toto Africans Vs Mwadui (CCM Kirumba – Mwanza), na siku ya jumapili Young Africans Vs Coastal Union (Taifa – Dar es salaam).
Ratiba kamili hii hapa, angalia mechi zote za timu yako hapo chini…
Vodacom Premier_Page_1
Vodacom Premier_Page_3
Vodacom Premier_Page_4
Vodacom Premier_Page_5
Vodacom Premier_Page_6
Vodacom Premier_Page_7
Vodacom Premier_Page_2


No comments:

Post a Comment

Popular Posts