Wednesday, August 19, 2015

HAWA NDIO KAUZU FC SHANGILIA YAO HII HATARI NDANI YA NDONDO CUP ( UWANJA WA BANDARI- TANDIKA)


Kauzu 31Pambano kati ya Kauzu FC dhidi ya Sifa United ni moja kati ya mechi zilizoweka historia ya kushuhudiwa na umati mkubwa wa mashabiki katika michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup ambayoinaendelea na sasa ikiwa kwenye hatua ya 16 bora. Jana mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Bandari, Tandika na mechi hiyo kuwa burudani nyingine kubwa kwa wapenzi wa soka wa vitongoji vya jiji la Dar es Salaam.
Kauzu 17Kama ilivyo ada ya michuano hiyo pindi panapokuwa na mechi basi lazima kuwe na burudani nyingine nje ya uwanja kutoka kwa mashabiki wa timu zinazokuwa zikipambana uwanjani kusaka ushindi. Nje ya uwanja kunakuwa na timu nyingine mbili za ushangiliaji zikipambana kuhakikisha timu zao zinaibuka na ushindi kwa kuzishangilia mwanzo mwisho.
Kauzu 23Wakati mcheo wa jana ukiwa umepamba moto, kiliiingia kikosi cha ushangiliaji cha Kauzu FC ambacho kilichelewa kwa dakika chache na kukuta mchezo tayari umeshaanza kwa takribani dakika tano hivi.
Kauzu 19Baada ya timu hiyo ya ushangiliaji ya Kauzu FC kutinga uwanjani, uwanja wote ulilipuka shangwe kutokana na amshaamsha zilizofanywa na washangiliaji wa Kauzu FC ambao walikuwa wakiimba na kupiga ngoma zilizoonekana kuwakuna mashabiki wengi wa timu hiyo.
Kauzu 21Kubwa zaidi ni babu aliyekuwa akiongoza timu hiyo ya ushangiliaji. Mzee huyo alikuwa amejichora kwa rangi, amevalia msuli na amebeba kapu kubwa lilishonwa kwa majani maarufu kwa jina la ‘miyaa’.
Tofauti na watu wengi walivyodhani, mzee huyo alianza kuuzunguka uwanja mzima akipunga mkono kwa mashabiki wa timu hiyo ambapo kila alipopita na kupunga mkono ziliibuka shangwe za kutosha huku watu wakimshangilia kwa kupiga makofi.
Kauzu 23Mtandao huu ukataka kujua siri ya mzee huyo kuwa sehemu ya timu ya ushangiliaji ya Kauzu FC, kwa taarifa za haraka tu akasema yeye amekuwa sehemu ya timu hiyo kwa muda mrefu na anaipenda sana Kauzu FC kuliko timu nyingine yoyote ndio maana ameamua kuacha mambo mengine na kuibuka uwanjani kuongoza kikosi kizima cha ushangiliaji kuhakikisha Kauzu inaibuka na ushindi na kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts