Klabu ya Simba August 13 wamezungumza na waandishi wa habari katika Press Conference ambayo waliiandaa wao wenyewe, Simba
imezungumzia mchezo watakaocheza siku ya Jumamosi ya August 15 Uwanja
wa Taifa Dar Es Salaam sambamba na kuweka wazi juu ya hatma ya golikipa Ivo Mapunda na mshambuliaji Elias Maguli ni kweli wametemwa?
“Jumamosi
tarehe 15 timu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa
kirafiki na timu ya URA ya Uganda mchezo utachezwa Uwanja wa Taifa Dar
Es Salaam saa 10 jioni na timu ya URA inatarajia kuwasili mchana huu
kutoka nchini Uganda, maandalizi yote yameshakamilika”>>> Haji Manara
“Kila kitu
kipo sawa Simba inatarajia kuutumia mchezo huo kuwajaribu wachezaji
wake wawili wapya mshambuliaji mmoja na golikipa”>>> Haji Manara
“Elias
Maguli nafikiri kumbukumbu zetu zipo vizuri kabisa Elias Maguli
alisajiliwa huu ni msimu wake wa pili ambao utaanza mwezi wa nane kwa
mkataba wa miaka miwili ni mchezaji wa Simba mpaka hapa ninapo zungumza
ni mchezaji wa Simba kilichotokea ni kwamba wakati tukijiaandaa na
mchezo wa Simba Day katika orodha ya mwalimu ya wachezaji 22 aliowataka
jina la Elias Maguli halikuwemo”>>>Evans Aveva
“Jina lake
halikuwepo kwa vigezo ambavyo mwalimu anavijua na sisi kama wanasimba
na stake holder wa mpira siku zote mmekuwa mkipiga kelele viongozi hasa
wa vilabu vya Simba na Yanga mmekuwa mkiingilia majukumu ya walimu sisi
tukaona tuheshimu hilo pamoja na kwamba Elias Maguli tulimsajili kwa
matumaini makubwa”>>>Evans Aveva
“Lakini
mwalimu alipokuja akaona uwezo wa Elias Maguli ni mdogo kwa hiyo katika
ile mechi ya Villa Elias Maguli hasishiriki kinachofuata baada ya hapo
ni maongezi pamoja na viongozi wa Simba kujua hatma yake, Ivo Mapunda ni
mchezaji ambae kamaliza mkataba wake alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja” Evans Aveva
“Sisi
tuliona ni jambo jema sana kuendelea na Ivo kwa sababu ya uwezo
aliouonyesha msimu uliopita hivyo kamati ya usajili ilianza kufanya
mazungumzo ya kina ikafikia mahali ambapo ikaonekana Ivo ataendelea kuwa
mchezaji wa Simba Sports club katika kipindi kinachokuja”>>>Evans Aveva
“Mazungumzo
yalifikia hitimisho na wakakubaliana Ivo atakuja kusaini mkataba na
klabu yetu ya Simba mpaka hivi ninavyo zungumza ni kwamba ni bahati
usajili umesogezwa mbele kwa hiyo bado tuna muda lakini mpaka hapa
ninavyozungumza Ivo bado hajaonekana kuja kusaini mkataba Simba hivyo
jukumu hili limerudishwa tena katika kamati husika na maadam usajili
umesogezwa mbele na Ivo yupo bado Dar tutatoa majibu”>>>Evans Aveva
No comments:
Post a Comment