Thursday, August 6, 2015

DIAMOND APATA MTOTO WA KIKE BAADA YA ZARI KUJIFUNGUA

MTOTO WA ZARI
Mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akiwa amembeba mjukuu weke. Kulia ni Zari
-599Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’.
MPENZI wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Zarinah Hassan ‘Zari’ amejifungua mtoto wa kike leo alfajiri saa 10: 40 jijini Dar es Salaam. Mtandao huu umeongea na Meneja wa kimataifa wa Diamond Platinumz, Salam Sharaf ambaye amethibitisha taarifa hizo na kusema Zari bado yupo hospitali mpaka sasa.
-1541Kutokana na usumbufu aliodai unaweza kutokea, Salam hakuweka wazi hospitali aliyojifungulia Zari. “Ni kweli Zari kajifungua mtoto wa kike majira ya saa 10 alfajiri leo, lakini kutokana na usumbufu unaoweza kujitokeza kwa sasa siwatajii hospitali aliyojifungulia mpaka hapo baadaye” Alisema Salam.
Kupitia akaunti za mitandao ya kijamii, Diamond Platnumz amemkaribisha duniani binti yake huyo aliyemuita Tiffah kwa kuandika hivi: Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya moyo wangu… karibu kwenye ulimwengu
Maneno hayo yaliambatana na picha ya mama yake mzazi aitwaye, Sanura Kassim ‘Sandra’ anayeonekana akiwa amembeba mjukuu wake hospitali. Pembeni ya picha hiyo yupo Zari.
DIAMOND
Mtandao huu unatoa pongezi wa Diamond pamoja na Zari kwa kupata mtoto wa kike.Diamond-and-Zarina-Hassan

Zari
Staa wa Bongo Fleva ambaye jina lake limebeba uzito mkubwa Afrika, Diamond Platnumz anayo furaha kushare na sisi hii good news… Post yake Instagram inasomeka hivi >>> ‘My mom’s face it’s enough to Express how i feell😍… Welcome to the world @princess_tiffah👼 Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya Moyo wangu😍… karibu kwenye ulimwengu@princess_tiffah‘ >>>> @
-599

No comments:

Post a Comment

Popular Posts